Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania ieingia mkataba mpya wa udhamini a jezi na kampuni ya usafirishaji wa anga ya Fly Emirates . Mkataba huo utaanza kufanya kazi msimu ujao ambao Real watavaa jezi zenye nembo ya Emirates kwa muda wa miaka mitano .
Mkataba huu mpya unamaanisha kuwa Real itamaliza mahusiano yake na kuchezesha kamari za kwenye michezo ya huko Austria ya Bwin ambayo imekuwa ikidhamini Madrid kwa miaka sita iliyopita tangu mwaka 2007 ambapo Madrid ilikuwainapata Euro milioni 15 kwa mwaka .
Mkataba wa udhamini ambao Madrid imeingia na Emirates ni wa miaka mitano ambapo Emirates itawalipa Madrid Paundi milioni 25 kwa mwaka .
Mkataba huu utaofanya Real Madrid kuwa timu ya tatu kwenye orodha ya timu zinazodhaminiwa kwa fedha nyingi nyuma ya Manchester United wanaodhaminiwa kwa Euro milioni 33 na Fc Barcelona wanaodhaminiwa na Qatar Foundation kwa Euro milioni 30
No comments:
Post a Comment