Blogger Widgets Blogger Widgets

Tuesday, May 21, 2013

MR.NICE AZOMEWA NA MASHABIKI CLUB

Mr. Nice

TAKEU king a.k.a mr nice ambaye yupo nchi jirani ya kenya baada ya kupata shavu na Grandpa record, jumapili iliyopita alijikuta katika fedhea ya aibu baada ya mashabiki kupiga boooooo za kutosha baada ya kutoa kauli za kutowafurahisha mashabiki

Inshu ilikuwa hivi mr. nice alitoka siku hiyo na kuingia viwanja kwenda kula good time akajikuta amezama club moja inaitwa iClub kuna mchekeshaji mmoja wa kenya huwa anafanya show zake hapo basi Mc baada ya kumwona Mr. kidali Poo akabidi ampe shavu kwa kuwatangazia mashabiki kuwa kuna celebrity Mr.nice in da house hivyo mashabiki wakataka mr. nice asimame tu na kuwapungia mkono lakini cha ajabu mr.misifa ooh sor mr. nice akakataa kusimama wala kupunga mkono kwa fans wake nipo songombingo likampata kwa kula "buuuuuuuuuuuuh" za kutosha akaona isiwe tabu akasimama akapora microphone na kubwabwaja"amnilipi nyinyi nikipanda hapa kwenye jukwani nitashtakiwa mimi" watu wakazidi kuzomea na kumtaka dj. apige kitu cha "Mac Muga" cha Alli kiba Dj hakuwa na hiyana zaidi ya kukonga nyoyo za mashabiki, wakati huo huo inasemekana Mr. nice karudia tabia zake za zamani za kupanda mti kata mti(kupiga starehe) ambazo zilimfanya akapotea kwenye gemu baaada ya kufulia , mnyetishaji anazidi kubwabwaja kuwa jombaa baada ya kufanya vishow kadhaa akiwa na DNA sasa club na Bar za kenya zishaanza kumjua ye ni nani ni bata after bata mpaka kuku wanaona wivu!!...

No comments: