Blogger Widgets Blogger Widgets

Wednesday, February 27, 2013

CHAPISHO MAALUM

                                                   jay-z tour
kuna maswali huwa najiuliza kwa hawa wasanii wetu wa kitanzania huwa wakisikia wanashow maandalizi yao huwa yapi? au ndo hizo kwenda madukani na kuazima pamba plus kutuvalia singo batani wakati ukumbi wenyewe joto kali,juzi kati nilikuwepo kwenye hizi show zao wanazofanyaga maisha na bilicana yaani unaona kabisa kuwa hakuna maandalizi yoyote wanayofanya zaidi wanawaza kujenga matumbo msanii mkubwa unakazi ya kusema mikono juu mwanzo mwisho sasa watu tumelipa viingilio sio kusikia mikono juu pili mazingira mnayopigia show ni ndogo.imefika kipindi sasa tujaribu kuingia na bendi zinagonga beats zako afu kidume unaonyesha kwanini uliitwa msanii na sio blah blah afu huyo unasepa.
kuna msanii ningependa niweke jina kapuni, hivi umewahi kuona wapi msanii mkubwa mfano hawa wenzetu wa magaibuni anaingia na kuanza" eti kuna watu wanataka kunizomea"tuwapige booo" hivi unazani wakina jayz hawana watu wanaowachukia au bifu nao anao sema anajua yupo kazini  na kamwe haangalii vitu vidogo vidogo anaangalia ni vipi awakonge mashabiki wake acha wazomee au huyu msanii haangaliagi hata mpira inamaana wakina cr7 wangekuwa wanaacha kucheza nakuanza kujibishana na mashabiki wanaopiga booooo..hivi unategemea nini ukisema hivyo kuwa kuna watu wamekuja kuzoemea inamaana umewapa promo ya kuzomea na kuleta fujo,.mimi si mwandishi wa habari na wala si msanii ila naumia kuona music wetu hautaki kwendana na wakati uliopo nakumbuka miaka ya 90 ndo playback kwa sana lakini wasanii wa kitanzania mmeshindwa kubadilisha huo msimamo tumechoka kuona sura zenu na pamba za kukodisha tunataka show kama ya picha ya hapo juu kwani si mnamameneja so wanafanya kazi gani?

No comments: