- WABUNIFU 23 KUTOKA TANZANIA KUONYESHA UBUNIFU WAO
- SWAHILI FASHION WEEK KUSHEHEREKEA MIAKA MITANO
Onyesho kubwa la mitindo la Afrika Mashariki na kati linarajiwa kufanyika siku tatu mfululizo katika Hoteli ya Golden Tulip kuanzia tarehe 6, 7 na 8 Desemba, 2012 ikiwa ni mara ya tano tangu kuanzishwa kwake.
Swahili Fashion Week 2012 kwa ujumla itakutanisha pamoja wadau 50 katika tasnia ya Mitindo kutoka nchi zinazozungumza Kiswahili na nyengine kuweza kuonyesha ubunifu wao na kutoa mustakabali wa mwenendo wa tasnia ya mitindo katika ukanda huu.
“Mwaka tumekuwa kwa kiasi kikubwa, wabunifu 23 kutoka Tanzania wataweza kuonyesha ubunifu wao na wengine waliobaki ni kutoka nje ya Tanzania, ambao wote wataonyesha ubunifu wao katika jukwaa moja ukiachilia wabunifu 16 walionyesha ubunifu wao katika maonyesha ya Swahili Fashion Week yaliyofanyika Nairobi, Kenya, Oktoba 6, 2012” Alisema Meneja wa Swahili Fashion Week, Washington Benbella
Read more: BongoCelebrity
No comments:
Post a Comment