Blogger Widgets Blogger Widgets

Sunday, June 16, 2013

ALPHA BLONDY NA TARUS RILEY WAGOMA KUFANYA SHOW BAADA YA PROMOTA KUSHINDWA KUWALIPA MSHIKO WAO

Tarrus concert
Jana Ilikuwa ni moja kati ya show kubwa za regge kufanyika katika ukanda huu wa East Afika kwa sababu ilijumuisha regge ya kale(Alpha Blondy) na regge ya kisasa au ya vijana wa sasa(Tarus riley & Damarco) vile vile Ticket zilikuwa si za bei ya chini kwa hivyo vigezo unapata picha kamili kuwa show hiyo ingefanikiwa ingekuwa ni show kubwa zilizowahi kufanyika nchini kenya
Tarus Riley
Lakini kitumbua kiliingia mchanga baada ya Alpha blondy na Tarus kushindwa kupanda kwenye stage  mnyetishaji wetu alitupa udaku kuwa promota wa show hiyo alishindwa kufikia makubaliano na wakali hao baada ya wakali hao kutaka walipwe kwanza ndio wakafanye show lakini promoter ambaye alikuwa akishirikiana na Ghetto Radio ambao ndio walikuwa wakiipromoti show hiyo kushindwa kufanya hivyo,,

 hivyo ikawabidi Alpha Blondy Na Tarus pamoja na  Demarco kugoma nao kutoka kwenye vyumba vya Hotel waliyofikia mpaka kieleweke
IMG_20130616_030542.jpg
Kitendo hicho cha kutokutokea kwa wakali hao waregge kulifanya mashabiki kupandwa na hasira na kushindwa kuzizuia hasira zao baada ya kukaa kwa muda bila kuona Alpha wala Tarus kwenye stage ndipo walipoanza kurusha chupa pamoja na kushambulia vyombo vya music na wale walafi kama mimi mnyetishaji tukavamia kitu cha creti za mubia na vyakula acha tuogeleee kwenye bia mpaka mawio a.k.a mornile hakuna cha Alpha wala demarco kupanda kwa jukwaa

No comments: